Habari Za Un

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 8:36:12
  • More information

Informações:

Synopsis

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Episodes

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya methali “MTI WENYE MATUNDA NDIO HURUSHIWA MAWE”.

    06/02/2025 Duration: 01min

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “MTI WENYE MATUNDA NDIO HURUSHIWA MAWE”.

  • 06 FEBRUARI 2025

    06/02/2025 Duration: 11min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwakina inayotupeleka Havan Cuba ambapo mmoja wa walumbi wa lugha ya Kiswahili Jorum Nkumbi, ambaye pia ni mwandishi wa vitabu anayetumia sanaa ya uandishi wa vitabu kuitangaza lugha mama yake ya Kiswahili amezindua kitabu kipya hivi karibuni wakati wa kongamano la kimataifa la Kiswahili. Mengine tuliyokuandalia ni kama yafuatayo.Yerusalem Mashariki eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli ambako Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Tom Fletcher yuko ziarani na amepata shuhuda halisi za wanaokabiliwa na kufurushwa makwao. Mmoja wao ni Um Nasser ar Rajabi ambaye amemweleza kuwa Nimekuwa kwenye ndoa katika nyumba hii kwa miaka 50.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu mahitaji ya dharura ya ulinzi na mazingira magumu yanayokabili raia kwenye eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC lenye utajiri mkubwa wa madini, wakati huu uhasama ulioshika kasi tangu mwezi uliopita kati ya jeshi la serikali n

  • Tumetembea wiki mbili kufika kambini Bushagara lakini bado hapa si nyumbani - Mwamini

    05/02/2025 Duration: 03min

    Kutana na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi. Kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu imekuwa mtihani mkubwa kwa wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi. Kupitia video ya shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Flora Nducha anafafanua zaidi katika Makala hii.

  • Uhamishaji watu kwa lazima kutoka kutoka ardhi inayokaliwa sio sahihi - OHCHR

    05/02/2025 Duration: 01min

    Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa,(OHCHR) imesisitiza haja ya kusonga mbele kuelekea awamu inayofuata ya usitishaji mapigano huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wote waliokamatwa kiholela, kukomesha vita na kujenga upya Gaza, kwa kuheshimu kikamilifu sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu. 

  • 05 FEBRUARI 2025

    05/02/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama Goma DRC, na masuala ya haki za binadamu. Makala na mashinani inaturejesha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kufuatilia simulizi za wakimbizi wa ndani.Maisha yanarejea katika hali ya kawaida huko Goma baada ya siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FARDC) na waasi wa M23 mashariki mwa. Mwandishi wetu wa habari jimboni Kivu Kaskazini amesema kwamba shughuli zinaanza tena katika mji wa ziwa la Kivu, Goma, wakati M23 imechukua wilaya nyingi za mji mkuu wa Jimbo hili.Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesisitiza haja ya kusonga mbele kuelekea awamu inayofuata ya usitishaji mapigano huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wote waliokamatwa kiholela, kukomesha vita na kujenga upya Gaza, kwa kuheshimu kikamilifu sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu.Makala leo inakukutanisha na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC wal

  • M23 wasitisha mapigano

    05/02/2025 Duration: 01min

    Maisha yanarejea katika hali ya kawaida huko Goma baada ya siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FARDC) na waasi wa M23 mashariki mwa. Mwandishi wetu wa habari jimboni Kivu Kaskazini amesema kwamba shughuli zinaanza tena katika mji wa ziwa la Kivu, Goma, wakati M23 imechukua wilaya nyingi za mji mkuu wa Jimbo hili. Alikutana na Muhindo Kibwana muendesha pikipiki akiwa kwenye maegesho yake ya kazi, jina lake limebadilishwa kwa usalama wake.

  • 04 FEBRUARI 2025

    04/02/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kushuhudia sintofahamu na maombi ya wakazi wa Goma baada ya waasi wa M23 kutwaa mji huo. Mashinani tunakwenda Somalia na pia tunakuletea muhutasari wa habari.Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bruno Lemarquis, ametoa wito wa kufunguliwa haraka kwa Uwanja wa Ndege wa Goma. Amesema uwanja huu uliofungwa kutokana na mapigano kati ya vikosi vya jeshi la DRC na waasi wa M23 ni muhimu kwa usafirishaji wa misaada ya kibinadamu. Hospitali zimejaa na maelfu ya raia hawana msaada wa dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu na afya ya uzazi, (UNFPA), na la misaada ya kibinadamu na dharura (OCHA) leo yamesisitiza kuwa kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani kunawaacha mamilioni 'hatarini'. Hayo yakijiri tayari imefahamika kuwa Rais Donald Trump anaiondoa Marekani katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na pia kuacha k

  • UNFPA - Wakimbizi zaidi ya 18,000 wa Sudan sasa wanaishi katika kambi ya Korsi CAR

    03/02/2025 Duration: 17s

    Vita inayoendelea Sudan kwa zaidi ya miezi 18 sasa inaongeza wimbi la wakimbizi ndani na nje ya nchi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA. Shirika hilo linasema takriban wakimbizi 18,000 waliokimbia vita Sudan hivi sasa wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Korsi katika eneo la Birao, jimbo la Vakaga Katikati Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambako UNFFPA inawapatia huduma muhimu zikiwemo za aya ya uzazi. Flora Nducha anatujuza zaidi katika makala hii

  • Maandamano huko Goma DRC, wakimbizi waomba UN iwafikishie misaada

    03/02/2025 Duration: 03min

    Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi

  • Tutafute majadiliano badala ya kugawanyika - Guterres

    03/02/2025 Duration: 01min

    Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani. Anold Kayanda na maelezo zaidi.

  • 03 FEBRUARI 2025

    03/02/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC, na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na mashinani tunarejea DRC, kulikoni?Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi.Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani.Makala inatupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwenye kambi ya wakimbizi ya Korsi inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 kut

  • Hali ni tete mashariki mwa DRC, msaada wa kibinadamu haufikii wahitaji - Mashirika

    31/01/2025 Duration: 01min

    Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia. Selina Jerobon amefuatilia matamko ya mashirika hayo na kutuandalia taarifa ifuatayo. Janga la haki za binadamu katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) linaendelea kuzidi kuwa baya kutokana na ripoti zinazonyesha kuwa kundi la wapiganaji la M23 limeendelea kusonga kusini kuelekea Bukavu, imeeleza Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) leo Januari 31 mjini Geneva, Uswisi.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) katika taarifa iliyotolewa katika mji Mkuu wa DRC, Kinshasa, limesema licha ya juhudi hizo zinazoendelea ili kusaidia watu, kuongezeka kwa ghasia kumelazimisha IOM na mashirika mengine ya kibinadamu kusitisha operesheni katika maeneo yaliyoathirika zaidi, na hivyo kusitisha msaada wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu.Kwa upande wak

  • Umeme wa uhakika wanufaisha wanafunzi na jamii nchini Senegal

    31/01/2025 Duration: 03min

    Senegal, taifa lenye watu zaidi ya milioni 18.5 liko kwenye mwelekeo wa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme. Benki ya Dunia inasema kiwango cha kupata umeme kwenye taifa hilo sasa ni asilimia 84. Wakati huu ambapo asilimia zaidi ya 30 ya jamii za vijijini hazina huduma hiyo, serikali kwa kushirikiana na wadau kama vile Benki ya Dunia na sekta binafsi imechukua hatua na mabadiliko yameanza kuonekana. Je ni yapi? Assumpta Massoi anaelezea kwenye makala hii.

  • 31 JANUARI 2025

    31/01/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tutakuletea simulizi ya wakimbizi wa ndani nchini humo. Makala inatupeleka nchini Senegal na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni?Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia..Kutana na mkimbizi Masimango Mango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambaye kwa sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagara Goma jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC, anasema kwa hakika vita imemchosha na anacholilia ni amani ili arejee nyumbani na familiia yake.Makala tunakwenda Senegal, magharibi mwa AFrika ambako nishati ya umeme imeleta mabadiliko makubwa kwenye kijiji ambacho awali kiligubikwa na kiza nyakati za usiku.Na katika Zulaikha kutoka Afghanistan ambaye ana matumaini katika msimu huu wa baridi kutokana na msaada wa fedha kutoka Shirika la Marekani

  • Tumechoka na vita tunachotaka ni amani turejee nyumbani: Masimango Mango

    31/01/2025 Duration: 01min

    Kutana na mkimbizi Masimango Mango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambaye kwa sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagara Goma jimboni Kivu Kaskazini  Mashariki mwa DRC, anasema kwa hakika vita imemchosha na anacholilia ni amani ili arejee nyumbani na familiia yake. Flora Nducha na taarifa zaidi.

  • Jifunze Kiswahili: Maana ya neno “MAADHURA”

    30/01/2025 Duration: 53s

    Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “MAADHURA”

  • 30 JANUARI 2025

    30/01/2025 Duration: 10min

    Hii leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayotupeleka nchini Tanzania ambapo Chuo cha ulinzi wa amani kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ‘UNITA’ na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Operesheni za Ulinzi waliandaa mpango wa ufundishaji kuhusu ulinzi wa amani, Brigedia Jenerali George Itang’are ambaye Mkuu wa chuo hicho anaelezaIkiwa leo ndio siku ambayo Israeli ilitaka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA liwe limefunga shughuli zake Ukanda wa Gaza, Msemaji wa UNRWA Julie Touma amenukuliwa akisema hadi sasa hawajapokea mawasiliano yoyote rasmi ya jinsi ya kutekeleza sheria ya Bunge la Israeli, Knesset inayotaka waondoke.Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi wa dharura, CERF umetenga dola milioni 17 kufanikisha operesheni za kiutu nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mapigano makali huko Kivu kaskazini na Kivu Kusini yameacha mamia ya maelfu ya wakimbizi wakiwa na mahitaji makubwa ya kibinadamu.Na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jana Januari 29 w

  • UNEP: Mradi wa UNREDD umekuwa mkombozi kwa mazingira na kwa wakulima DRC

    29/01/2025 Duration: 03min

    Karibu nusu ya idadi ya watu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wanategemea misitu kwa chakula, nishati, afya, riziki na huduma za mfumo wa ikolojia kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP ambao ni takriban watu zaidi ya milioni 40. Kwa kulitambua hilo mradi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda bayoanuai huku ukipambana na umasikini UNREDD unaleta nuru kwa raia hususani mashariki mwa nchi hiyo. Ungana na Flora Nducha kwa ufafanuzi zaidi katika makala hii.

  • UNAIDS: Marekani yatangaza kurejesha ufadhili dhidi ya VVU

    29/01/2025 Duration: 02min

    Baada ya Serikali ya Marekani kutoa tangazo jipya sasa kwamba itaendelea kufadhili huduma zinazolenga vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi (UNAIDS) limeeleza kuupokea uamuzi huo kwa furaha na kuuita wa kuokoa maisha. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

  • 29 JANUARI 2025

    29/01/2025 Duration: 09min

    Hii leo jaridani tuanaangazia masuala ya ufadhili wa huduma za afya, na kilimo cha cacao nchini Liberia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Baada ya Serikali ya Marekani kutoa tangazo jipya sasa kwamba itaendelea kufadhili huduma zinazolenga vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na VVU na Ukimwi (UNAIDS) limeeleza kuupokea uamuzi huo kwa furaha na kuuita wa kuokoa maisha.Kilimo bora cha kakao huko Liberia kimemwondolea uchovu na kukosa kulala, mkazi wa kaunti ya Nimba, kaskazini mashariki mwa Liberia, baada ya mradi wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD nchini humo kumwezesha sio tu kugeukia kilimo, bali pia kuajiri vijana wengine na hivyo kufanikisha lengo la Umoja wa Mataifa la kuondokana na umaskini.Makala inatupeleka kwenye msitu wa bonde la mto Congo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC wa pili kwa ukubwa duniani unaofyonza kiasi kikubwa cha hewa ukaa, ambako mradi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda bayoanuw

page 1 from 5