Synopsis
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
Episodes
-
Machi nane siku ya kuangazia haki za mwanamke
12/03/2025 Duration: 10minKwenye makala haya tunaangazia Siku ya kimataifa ya wanawake, inayoadhimishwa kila mwaka Machi 8, siku hii hutumika kutambua mchango wa wanawake katika jamii na kupigania usawa wa kijinsia. Ni siku ya kusherehekea mafanikio ya wanawake katika nyanja mbalimbali kama vile siasa, uchumi, sayansi, na sanaa, huku ikihamasisha juhudi za kuondoa changamoto wanazowakabili wanawake, kama vile ubaguzi, ukatili wa kijinsia, na ukosefu wa fursa sawa.Kaulimbiu ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa kushirikiana ili kujenga jamii yenye usawa, ambapo kila mtu ana nafasi sawa ya kufanikiwa bila kujali jinsia yake. Katika dunia inayoendelea kubadilika, ni muhimu kuendelea kushinikiza sera na vitendo vinavyohakikisha wanawake wanapata haki zao kikamilifu.Siku hii hutumika kutoa wito wa kuchukuliwa hatua kwa serikali, mashirika, na watu binafsi ili kuunda ulimwengu wenye fursa sawa kwa wote.
-
Kenya : Mahakama ya madai madogo madogo
11/03/2025 Duration: 09minWakenya wameshauriwa kutochukua hatua mikononi iwapo wana mzozo wa malipo baina yao na watu wanaowadai. Hii ni baada ya maafisa wanahudumu mahakamani, mawakili na asasi za kijamii kufanya mkutano wa kueneza uwepo Wa mahakama hizo nchini Kenya huku wakiwahimiza raia kutumia korti hiyo ambayo inatatua kesi chini ya miezi miwili. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Haki ya wanahabari kutumia teknolojia ya AI
01/03/2025 Duration: 10minKatika hii ya kidijitali na inayobadilika kwa kasi, teknolojia ya akili mnemba (AI) imekuwa sehemu muhimu ya sekta mbalimbali, ikiwemo uandishi wa habari. Katika mkutano wa "Ubunifu AI kwa Mustakabali Endelevu wa Vyombo vya Habari" ulioandaliwa na Tamasha la Vyombo vya Habari Afrika kwa kushirikiana na taasisi ya Baraza Media Lab, wadau wa sekta ya habari walijadili kwa kina athari za AI katika tasnia hiyo ya wanahabari . Mkutano huo ulilenga kuelewa jinsi AI inavyoweza kutumiwa kwa uwajibikaji ili kuimarisha kazi ya wanahabari.Matumizi ya akili mnemba katika uandishi wa habari yanaweza kuboresha utendaji kazi wa wanahabari kwa njia mbalimbali. Kwanza, AI inaweza kurahisisha utafiti na uchambuzi wa taarifa kwa kasi zaidi, hivyo kuokoa muda wa wanahabari. Kwa mfano, AI inaweza kusaidia katika uchanganuzi wa data kubwa, kugundua mwenendo wa habari, na kutengeneza muhtasari wa matukio kwa haraka.Pili, AI inatoa fursa ya kuboresha uthibitishaji wa habari kwa kusaidia wanahabari kugundua habari za uongo au zilizo
-
Kenya haki raia mtoto wa kike kupata elimu
23/02/2025 Duration: 09minShiniko zaidi zinazidi kutolewa kwa mtoto wa kike kuendelea kuwepeza uwezo wa kujiendeleza kimasomo, licha ya kwamba wengi wao sasa wapo katika nafasi nzuri kimasomo ukilinganisha na awali. Katika makala haya Benson Wakoli, amezungumza na wanafunzi wa kike kufahamu lengo lao kujiendeleza kimasomo.
-
Kenya : Vijana wa Kenya hawana ajira
19/02/2025 Duration: 09minNchini Kenya kwa mjibu taasisi ya twakwimu za serikali vijana millioni 3.5 hawana ajira, kumbuka idadi hii inawewa kuwa ya juu zaidi . Vigezo kadhaa vikihusishwa na ukosefu huo wa ajira, wakati huu serikali nayo ikisema ipo katika juhudi za kuhakikisha vijana wapata ajira.Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Serikali ya Uganda yapata shinikizo kumwachia kiongozi wa upinzaji Kizza Besigye
18/02/2025 Duration: 09minSerikali ya Uganda inapata shinikizo kutoka kwa wapinzani na watetezi wa haki za binadamu kumwachia huru mwanasiasa mkongwe Kizza Besigye anayekabiliwa na mashaka katika Mahakama ya kijeshi ambaye kwa siku kadhaa sasa amegoma kula akiwa gerezani, hali ambayo imedhoofisha afya yake.Tulimuuliza msikilizaji anazungumzia vipi masaibu yanayomkumba Besigye na anafikiri ni kwanini inachukua muda kuihamisha kesi ya mwanasiasa huyo kutoka Mahakama ya kijeshi kwenda kwenye Mahakama za kiraia ?
-
DRC : Haki ya raia wa Goma baada ya waasi wa M23 kuwasili eneo hilo
06/02/2025 Duration: 09minKatika makala haya tunazama kuangazia hali ya kibinadamu kule Goma baada ya waasi wa M23 kuwasili katika mji huo.Je hali ya kibinadamu ipo je baada ya waasi wa M23 kuwasili Goma. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Africa : Serikali zinaendelea kukiuka haki za raia
28/01/2025 Duration: 10minShirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Human Right Watch limechapisha taarifa lituhumu serikali za Africa namna gani zimeshindwa kulinda haki za raia wake. Katika makala haya Benson Wakoli amezungumza na maafisa kutoka Human Right Watck kuelewa hali kamili/.Skiza makala haya kuelewa zaidi.
-
Juhudi zilizopo kuondoa hukumu ya kifo kwenye nchi barani Afrika
21/01/2025 Duration: 10minKatika nchi nyingi barani Afrika, adhabu ya kifo inasalia kuwa suala tata, ikiwa imejikita katika mifumo ya kisheria na kijamii. Licha ya mjadala kuhusu ufanisi na maadili yake kuendelea, wanaharakati wa haki za binadamu wanajitahidi kuhakikisha kufutwa kwa adhabu hiyo, wakisisitiza haki ya msingi ya kuishi. Ulaya tayari imeondoa adhabu ya kifo, ikitoa mfano wa mfumo wa haki unaolenga marekebisho badala ya adhabu kali.Kwenye makala haya tumeangazia juhudi hizo kuondoa adhabu hiyo .
-
Kenya: Uhuru wa kutumia mitandao ya kijamii na mipaka yake
09/01/2025 Duration: 10minSiku ya Jumatatu asubuhi Vijana wanne kati ya 6 waliotekwa nyara katika wiki za hivi majuzi waliachiliwa huru, saa chache kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanyika kupinga kutoweka kwao. Billy Munyiri Mwangi na Peter Muteti waliungana na familia zao huko Embu na Nairobi, mtawalia, baada ya kuzuiliwa kwa zaidi ya wiki mbili ilhali Rony Kiplangat alipatikana katika kaunti ya Machakos naye Benard Kavuli akapatikana katika maeneo ya Kitale magaribi mwa nchi. Katika makala Jua haki zako, tunaangazia huru wa kutumia mitandao ya kijamii na katika kutumia mitaoa hiyo kuna mipaka yake. Je nchini Kenya hatua zipi zinafaa kuchukuliwa ikiwa mshukiwa atapatikana na hatia ya kukiuka huru ywa mitandao ya kijamii.
-
Dunia:Haki za wanawake na Ukomeshaji wa visa vya mauaji
30/12/2024 Duration: 09minMakala jua haki zako leo yataangazia haki za kina dada,changamoto wanazopitia na nini wanaharakati wanafanya ili kuhakikisha visa vya dhulma vinaripotiwa kwa wakati na haki inatendeka.Kumbuka killa mwaka, kuanzia tarehe 25 Novemba hadi 10 Disemba, dunia inaungana kwa pamoja kutambua changamoto kubwa zinazowakumba wanawake na wasichana, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia, ukatili wa kifamilia, na vitendo vingine vyote vya ubaguzi na dhuluma.
-
Kenya : Akili dada na Juhudi zake za kuinua maisha ya mtoto wa kike
18/12/2024 Duration: 10minJoy Zawadi, mkurugezi mkuu wa shirika la Akili Dada, linalopigania haki za mtoto wa kike alikiti chini na Benson Wakoli, kujadili juhudi wanazofanya kuinua mtoto wa kike nchini Kenya. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
Kenya : Akila Dada mstari wa mbele kutetea haki za mtoto wa kike
17/12/2024 Duration: 10minHaya ni awamu ya pili ya makala haya, ambapo Joy Zawadi afisa Mtendaji kutoka shirika la Akili Dada, anaendelea kujadili namna gani haki za mtoto wa kike zinaweza kuheshimiwa. Kufahamu mengi zaidi skiza makala haya.
-
DRC : Mchango wa AU kumaliza mizozo Africa
16/12/2024 Duration: 10minMoses Balagisi, afisi kutoka shirika la umoja wa Africa linaloshirikiana na masharika ya kiraia, kuhakikisha uongozi wa juu wa AU unaskiza kilio cha raia wa chini, analeza namna gani wanahakikisha hilo linafanyika. Kufahamu mengi zaidi, skiza makala haya.
-
Kenya :Madaktari watishia kugoma tena tarehe 22 Disemba
09/12/2024 Duration: 10minWahudumu wa afya nchini Kenya wanaitaka serikali kuwatuma kazini wanafunzi na wahudumu wa afya mara moja na kufuta malimbikizo ya mishahara ya madaktari kulingana na Makubaliano ya Pamoja ya 2017. Wahudumu wa afya ambao wamehudumu kwa miaka minne chini ya kandarasi katika taasisi za afya ya umma wanadai ajira ya kudumu ambayo walikuwa wamehakikishiwa na serikali ya Kenya kufuatia miaka mitatu ya huduma.
-
DRC : Haki ya mtoto kupata elimu na vizingiti vinavyochangia
12/11/2024 Duration: 10minKatika makala haya tunajadili haki za mtoto kupata elimu nchini DRC, hapa mkuu wa chuo cha walumu cha ISP, Butua Balingane anafafanua vizingiti vya mtoto kupata elumu nchini DRC. Kufahamu mengi skiza makala haya.
-
DRC : Haki ya wanawake kupata elimu
05/11/2024 Duration: 10minNchini DRC, kumeripotiwa upungufu wa watoto wa kike katika kupata elimu, hili likidaiwa kuchangiwa na tamaduni zilizopitwa na wakati. Katika makala haya basi Butua Balingane, mkurugezi wa chuo kikuu cha walimu cha ISP, Goma ambaye anasimulia masaibu anayopitia mtoto wa kike nchini DRC kupata elimu. Skiza makala haya kufahamu mengi zaidi.
-
Kenya : Wanawake 97 wauawa kwa kipindi cha miezi tatu
05/11/2024 Duration: 09minNchini Kenya, idara ya polisi imekiri kwamba wanawake 97 wameuawa kwa kipindi cha miezi 3, baadhi miili yao ikipatikana imenyofolewa. Ni visa ambayo vimesababisa viongozi wa ngazi ya juu akiwemo rais William Ruto, ambaye ametoa agizo wa asasi za uchunguzi nchini humo kuwasaka na kuwachukulia hatua wale wote ambao wamehusika katika visa hivyo. Kwenya makala haya tunazama kujadili kile kinachoendelea nchini Kenya, ambapo mtaalamu wa maswala ya jamii bi Carolina Situma anaeleza nini kimechangia mauwaji haya.
-
Kenya : Visa vya raia kutekwa yaongezeka
25/10/2024 Duration: 09minNchini Kenya, visa vya raia kutekwa na kisha baadaye kuachiliwa au kupatikana wameuawa vinazidi kuongezeka, visa kadhaa vikiendelea kugonga vichwa vya habari. Katika Makala haya George Ajowi angaazia visa hivi na jinsi mkuu wa polisi nchini Kenya alikosa kufika mahakamani kueleza walipokuwa baadhi ya wakenya waliotekwa.
-
Hatua zilizopigwa katika kumuinua mtoto wa kike
24/10/2024 Duration: 10minKatika muendelezo wa makala kuhusu siku ya mtoto wa kike duniani, tunaangazia vyanzo vya visa vya unyanyasaji wa watoto wa kike na hatua zilizopigwa na mashirika mbalimbali katika kuifanya sauti ya mtoto wa kike kusikika.