Jua Haki Zako

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:58:42
  • More information

Informações:

Synopsis

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episodes

  • Kenya: Haki ya matumizi ya vyombo vya dijitali

    10/06/2025 Duration: 10min

    Kadri Afrika inavyozidi kuingia katika ulimwengu wa  kidijitali, kila siku mamilioni ya watu wanaingia mitandaoni—kutafuta taarifa, kuwasiliana, kufanya biashara na hata kushiriki mijadala ya kisiasa. Lakini swali kuu ni Je, watu wote wanaelewa haki zao katika mazingira haya mapya ya kidijitali? Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Kenya : Haki ya wanaume na wanawake

    03/06/2025 Duration: 10min

    Kwenye makala haya tunaendeleza mahojiano yetu na Njeri mwangi mwanaharakati wa kutetea haki za kijisia Njeri mwangi Skiza makala Kufahamu mengi

  • Kenya : Harakati za kutetea jinsia

    31/05/2025 Duration: 10min

    Nchini Kenya, harakati za kutetea njisia inazidi kushika moto mwanaharakati Njeri Mwangi, akiendelea kuhamasisha raia. Skiza makala haya kufahamu mengi.

  • Amnesty International : Saudi Arabia inawanyanyasa wafanyakazi wa nyumbani

    23/05/2025 Duration: 09min

    Shirika la Amnesty International imeitaka serikali ya Kenya pamoja na ile ya Saudi Arabia kushiriiana na kuweka mikakati ya kuhakikisha haki za raia wa Kenya wanaofanya kazi katika mataifa ya Ugaibini hazitatiziki. Katika ripot iyake Amnesty imesema kuwa wanawake wanaofanya kazi za nyumbani huko Uarabuni wanapitia mateso za kijinsia, kunyanyashwa kimapato na hata kuuawa.

page 2 from 2