Synopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodes
-
Afueni kwa wanawake wanaokatwa matiti yao kutokana na saratani
02/11/2025 Duration: 09minKila mwezi wa Oktoba, ulimwengu huadhimisha Mwezi wa Uhamasishaji wa Saratani ya Matiti, lengo kuu likiwa kuhamasisha vipimo vya mapema ili kupunguza hatari ya ugonjwa huu na kutafuta msaada wa kifedha kwa ajili ya utafiti kuhusu saratani ya matiti. Inakadiriwa kuwa, wagonjwa wapya zaidi ya milioni 2.3 wa saratani ya matiti hugunduliwa kila mwaka, kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani. Wengi wa wanawake waliopatwa na saratani hii walilalzimika kukatawa titi moja au yote mawili ili kuokoa maisha yao, na hivyo kupoteza kiungo muhimu cha mwili.
-
Kabla kuchagua,kununua mafuta ya kupikia ,zingatia mambo hayo
30/10/2025 Duration: 10minMafuta ya mzeituni, alizeti, mafuta ya nazi,mafuta ya mawese ni baadhi ya mafuta kula ambayo yanapendekezwa kutokana na namna yanavyotengenezwa. Mengi hutengenezwa kwa kukamuliwa ,bila kuongezwa kemikali bila kutumia joto,hivyo ubora wake ni wa juu. Mafuta haya hata hivyo ni ya bei juu sana na watalaam wanashauri badala ya kuchagua mafuta ambayo si mazuri na ambayo yanaweza kuongeza mafuta ya Cholesterol mwilini na kusababisha matatizo ya afya ,machaguo mbadala ni mafuta ya uto . Mafuta haya yanaweza kutokana na mimea au mbegu. Mfano ni mafuta ya Parachichi,Karanga na hata Canola. Aidha watalaam wanatoa tahadhari kuwa ukitumia mafuta yako kupika ,usipende kuyarudia au kutumia kwa zaidi ya mara moja na usiyaweke mahali wazi maana yanayoweza kugeuka mabaya bila wewe kufahamu.
-
Yafahamu makundi tofauti ya mafuta ya kula,ubora ,madhara na matumizi yake.
15/10/2025 Duration: 09minKuanzia yale ya nazi hadi mizeituni, mboga hadi kanola, parachichi hadi mafuta ya wanyama maswali yameibuka kuhusu tunajuaje yapi mazuri ya kutumia, na ikiwa tunapaswa kuepuka yoyote yale kabisa Watalaam wa afya wanahoji mafuta ni kiungo muhimu katika mwili wa binadaam kwa kuwa huchangia madini muhimu na pia husaidia utendakazi wa viungo muhimu mwilini. Hata hivyo wanashauri mafuta kutumika kwa kiasi ili kuzuia mwili kujilimbikizia mafuta haswa ya Cholestrol ambayo yanaweza kusababisha mishipa ya kupitisha damu kuziba ,kusababisha saratani,shinikizo la damu na magonjwa ya moyo Katika orodha ya mafuta,kuna mafuta yanayotokana na mimea ,wanyama na yale yanayozalisha viwandani maarufu kama Trans Fats Maamuzi ya kutumia mafuta gani ,hata hivyo yanategemea ubora wake ,kazi ya mafuta na mapishi ya mtu Mafuta ya wanyama japo ni asilia yanapaswa kutumika kwa kiasi kidogo mno . Mafuta ya uto haswa ya mimea ni mazuri ila yanaweza kuharibika ikiwa utachanganyika na hewa ya oksijeni au yanapotumika kwa kurudiwa rudiwa
-
Masaibu ya wakaazi wa kisiwa cha Ndeda nchini Kenya wanaokosa vyoo vya kutosha
09/10/2025 Duration: 09minMwongozo wa shirika la afya duniani,WHO kuhusu usafi,unapendekeza choo kimoja kinaweza kutumika na watu 20 ila katika kisiwa cha Ndeda ndani ya Ziwa Victoria ,watu zaidi ya elfu 2 wanachangia vyoo vitano
-
Vipimo vya afya kabla ndoa vitakusaidia kuchukua maamuzi sahihi ya afya
03/10/2025 Duration: 09minKama kuna kipindi watu wengi huwa tumbo joto, ni kusubiri matokeo ya kipimo cha HIV au magonjwa mengi ya zinaa.Au kuambiwa huna uwezo wa kizazi. Hata hivyo unapofanya vipimo hivyo itakuokoa kufanya makosa ambayo yanaweza kuathiri familia yako baadaye. Ikiwa utapima baadhi ya vipimo hivi muhimu utaweza kujipanga kifedha na kuchagua matibabu ambayo yanaweza kutatua changamoto za afya ambazo pengine umekutwa nazo.
-
Je unafahamu vipimo vya afya unavyohitaji kupima kabla kufunga ndoa?
24/09/2025 Duration: 10minWatu wengi wanapokaribia kufunga ndoa,hujukumika kufanya vipimo vya virusi vya HIV .Wengi hufanya kipimo hicho si kwa sababu wanajua umuhimu wake bali ni kwa sababu ya ulazima kabla kufunga harusi haswa za Kikristo. Hata hivyo watalaam wa afya wanasema kuna vipimo tele ambavyo ni muhimu pia na vinahitajika kufanywa kabla ndoa. Mwanasaikolojia Naomi Ngugi anasema kando na kipimo cha HIV,kuna kipimo cha Rhesus Factor ambayo kama mtu na mwenzake hana ufahamu ,wanaweza kupata shida ya kuharibika mimba. Kuna pia kipimo cha Genotype kubaini uwepo wa ugonjwa kama Selimundu ,Hepatitis B, Hepatitis C au homa ya ini,vipimo vya Magonjwa sugu, Magonjwa ya akili na Vipimo vya uzazi kubaini ubora wa mbegu za kiume na matatizo ya mirija kuziba upande wa wanawake. Vipimo hivyo vinaweza kugharimu ndoa iwapo wanandoa hawataweka wazi.
-
Je unafahamu namna vyakula unavyokula njiani au hotelini vinaandaliwa vipi?
20/09/2025 Duration: 09minVyakula vinavyoandaliwa nje ya jikoni kwangu huwezi kufahamu viwango gani vya usafi vimezingatiwa Unapoaumua unakula kwa mama nitilie ni vigezo gani unaweza ukaweka ili kuhakikisha unalinda afya yako? Alfred Lobawoi kwenye makala haya ,amewahoji wauza vyakula na walaji kujua mtazamo wao
-
Nini kifanyike kuwezesha Mipango ya bima ya afya barani Afrika
09/09/2025 Duration: 10minJuhudi za serikali za Afrika kuja na mikakati ya kutoa huduma za afya kwa raia kupitia mipango ya bima ya afya ya kitaifa zimekabiliwa na changamoto za utekelezaji,ufisadi na mifumo isiyo thabiti. Watalaam wa afya sasa wanapendekeza mipango hiyo ya afya iwe kwenye mipango ya kitaifa ya kila mwaka,ikiwa na mwongozi kamili kuhusu huduma gani serikali itatoa kwa raia na kwa kiasi gani. Aidha watalaam wanashauri mipango hiyo iwe inaendana na mahitaji ya kila jamii kwa kuwa serikali nyingi kwa sasa hazina uwezo wa kutoa huduma zote kwa raia Isitoshe,mifumo inyopunguza uvujaji wa raslimali za umma ni muhimu
-
Utengano wa familia unaweza kuleta shinikizo la damu au kisukari
02/09/2025 Duration: 10minWanadamu ni viumbe ambao hukamilika wanapokuwa kwenye jamii ambapo wanaweza kuelezea hisia zao,kujihisi wanathaminiwa na wana mchango kwa wengine. Mambo hayo yanapokosa,inaweza kuwa chanzo cha matatizo ya kiafya.Na hii ni hali ambao hukuwa nao wakimbizi ambao wametenganishwa na wapendwa wao. Katika kambi ya Kakuma iliyoko kaunti ya Turkana,kaskazini mwa Nchi ya Wakenya,tulizungumza na wakimbizi ambao walilazimika kutengana na wapendwa wao kwa sababu ya migogoro ya kifamilia,ukoo na hata vita. Ingawa wamepata makao katika kambi ya wakimbizi bado maisha yao hayajakamilika . Wengi wameishi kwenye hali ya upweke,huzuni na kiwewe na kupata matatizo ya kiafya yakiwemo matatizo ya afya ya akili. Aidha kuna wale ambao wamepatwa na maradhi kama shinikizo la damu ,kisukari,ukosefu wa usingizi na chanzo ni matatizo ambayo wamekumbana nao katika kambi,ugumu wa maisha bila watu walio karibu nawe ambao unaweza kuzungumza nao na kuliwazana. Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC pamoja na shirika la msalaba mwekun
-
Utapiamlo unaweza kukusababishia Diabetes aina ya 5 wameonya watalaam wa afya
26/08/2025 Duration: 10minHivi karibuni watalaam wa afya pamoja kwa ushirikiano na shirikisho la ugonjwa wa kisukari duniani,wamethibitisha uwepo wa Kisukari aina ya tano ambao unahusishwa na utapiamlo Aina hii ya kisukari huathiri watu ambao hawakupata lishe bora wakiwa watoto na kuathiri ukuaji wa kongosho inayozalisha Insulin inayodhibiti sukari mwilini. Aidha kisukari aina ya tano inaweza kuwapata watu ambao wamekumbwa na njaa kwa muda mrefu ,kufanyiwa operesheni ambayo inafanya mtu kupungua mwili kwa kiasi kikubwa.
-
Unachohitaji kufahamu kuhusu ugonjwa wa Pneumonia unaoshambulia mapafu yako
21/08/2025 Duration: 09minWatu wengi hudhani kuwa Pneumonia husababishwa na baridi kuingia kwenye kifua lakini watalaam wanasema chanzo cha Pneumonia ni vimelea kushambulia mapafu na mfumo wa kupumulia Watalaam wa afya wanasema ndani ya wiki moja, mtu aliye na Pneumonia hugundulika kwa kuwa anapata ugumu wa kupumua au hata kukosa hewa.
-
Kwa nini ni muhimu kuongeza uwekezaji bunifu katika afya ya watoto
12/08/2025 Duration: 10minHali ya afya ya watoto haswa katika mataifa ya Afrika imeendelea kuzorota huku kukiwa na ongezeko la visa vya utapiamlo mbaya,ukosefu wa lishe na uhaba wa chanjo muhimu Taasisi zinazojikita kwenye afya ya watoto zinaonya kuwa punguzo kwenye ufadhili kwenye afya ya watoto utaathiri afya ya jamii kwa jumla. Pengo hili limetokana na ongezeko la mizozo na uchumi wa dunia uliotetereka tangu wakati wa janga la Uviko 19,hali hii ikipunguza msaada wa kibinadaam na kushurutisha mataifa kuwekeza kwenye maswala yanayoenekana muhimu zaidi Daktari Ahmed Ogwell afisa mkuu mtendaji wa shirika la VillageReach, anashauri kuwa uwekezaji bunifu katika kitengo hiki cha afya ni muhimu. Dkt Ogwell anapendekeza kuwa wakati huu mataifa yanapokabiliwa na punguzo kwenye ufadhili wa kigeni ni muhimu kwa mataifa kuziba mapengo ya ubadhirifu wa pesa za umma na kuwekeza kwenye miradi ambayo inakubalika kwenye jamii na isiyo ya gharama ya juu. Hii itahakikisha kuwa mataifa ya Afrika hayawi mataifa tegemezi kwa jamii ya kimataifa ambayo
-
Watalaam waonya ongezeko la visa vya H pylori katika maeneo ya mijini
05/08/2025 Duration: 10minH pylori isipotibiwa inaweza kugeuka kuwa saratani ya tumbo ,watalaam wameonya Katika makala haya,tunaangazia sababu ambazo zinaweza kuchangia mtu kupata maambukizo ya H pylori na matibabu yake. Matibabu yake kwa mujibu wa daktari Alex Mungala anayehudumu jijini Nairobi yanaweza kukabiliwa na usugu wa vimelea ,ni ghali na si rahisi kupatikana katika vituo vya afya vya daraja la kwanza.
-
Ukiwa utatembea hatua elfu saba kila siku unaweka magonjwa hatari mbali
29/07/2025 Duration: 10minUtafiti uliofanywa wa shirika la utafiti wa afya Lancet Public Health umebaini hatua elfu 7 kila siku unapunguza hatari ya kupatwa na magonjwa ya Saratani,Kisukari,magonjwa ya moyo, shinikizo la damu,sonona na kupoteza kumbu kumbu Kwa mujibu wa shirika la afya duniani ,WHO,mazoezi ya kudumu dakika 150 kila wiki au mazoezi makali ya dakika 75 ni mkakati wa kuimarisha afya. Katika makala haya nimejiunga na kundi la Nairobi Walk Movement,tawi la Buru Buru ambalo limejitoa kufanya matembezi ya kuanzia kilomita 10 hadi 20 na wakati mwingine hadi 40 kila Jumamosi asubuhi au Jumapili alasiri kuanzia saa tisa na nusu. Kundi hili pia limejisajili kwenye kundi la kuhesabu hatua ambazo kila mtu hutembea kila siku ,hatua hizo zikihesabiwa kutumia application maalum ya kuhesabu hatua,lengo likiwa hatua hadi elfu 10 kila siku. Kushindana kwa kuhesabu hatua kila siku umekuwa mchezo ambao huwatia moyo Wanachama hao wameelezea faida nyingi kutokana na kujiunga kwenye kundi hilo na kushiriki matembezi. Wapo waliokuwa na wa
-
Watalaam waonya kukaa muda mwingi kunaweza kukusababishia kifo cha mapema
23/07/2025 Duration: 10minKukaa kwa zaidi ya saa sita mfululizi kila siku inaweza kukuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa ya uti wa mgongo,kisukari,shinikizo la damu na kifo cha mapema
-
Baadhi ya hospitali nchini Kenya zinazalisha chakula kuwalisha wagonjwa
15/07/2025 Duration: 10minKatika mkakati wa kuboresha lishe,hospitali zinatumia vipande vya ardhi zao kukuza chakula kuwalisha wagonjwa wao
-
Serikali ya Kenya yazingatia afya ya akili miongoni wa vikosi vya usalama
10/07/2025 Duration: 09minWaziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema polisi wenye changamoto za afya ya akili hawatafukuzwa kazi bali watapewa matibabu stahiki Kumeshuhudiwa hivi karibuni visa vya polisi kutumia silaha zao visivyo na utendakazi wao kukosolewa na raia pamoja na wanaharakati wa haki
-
Je ni muda wa nchi za Afrika kujadili huduma ya kusaidiwa kufa ?
02/07/2025 Duration: 10minHivi majuzi bunge la Uingereza limepitisha mswada wa kuhalalisha huduma ya kusaidiwa mtu kufa Huduma hii itatekelezwa katika hospitali chini ya usimamizi wa wahudumu wa afya ,kwa watu wazima wanaougua magonjwa yasiyopona . Watalaam wa afya wanasisitiza kuwa hatua hiyo sharti mgonjwa kuridhia bila kushinikizwa .
-
Sera ya Kenya kuhakikisha raia wake wanafanya mazoezi kila mara
25/06/2025 Duration: 10minTakwimu zinaonesha watu wengi kupatwa na magonjwa yasiyoambukizwa kutokana na kuishi bila kufanya mazoezi na kula vibaya Sera hii itatoa mwongozo wa taasisi za serikali na binafsi kuweka mikakati ya kuruhusu mazoezi ya kila mara wakati wa kazi au nje ya kazi
-
Mwili wako unavyowasiliana kupitia utendakazi wake na kukupa onyo kukiwa tatizo
20/06/2025 Duration: 10minKila siku mwili wako hukuzungumzia na ni jukumu lako kusoma mwili wako na kuelewa unasema nini au unakuonya kuhusu nini Baadhi ya matatizo ambayo unaweza kujiepusha nayo ni matatizo ya afya ya akili ,kufeli viungo muhimu au mifumo yako ya afya. Na ili kuhakikisha mwili wako unazungumza na kutoa taarifa iliyo sahihi kuna baadhi ya vitu unaweza kufanya kwa mfano kupata muda wa kutosha kulala,kupata lishe bora na kufanya mazoezi