Synopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodes
-
Uhusiano wa karibu kati ya matatizo ya tezi koo na afya yako ya akili
12/06/2025 Duration: 10minMatatizo ya tezi koo yanaweza kujidhirisha kwa dalili kama vile msongo wa mawazo,kukosa usingizi,kiwewe na mtu kukosa ari ya chochote maishani Katika makala haya ,tunamtambulisha Daktari Violet Oketch anayesimamia kitengo cha afya ya akili katika hospitali kuu ya rufaa nchini Kenya ya Kenyatta. Daktari Violet anafafanua ufungumano kati ya matatizo ya tezi koo na matatizo ya afya ya akili. Aidha afisa mkuu mtendaji wa kikundi cha kuhamasisha kuhusu matatizo ya tezi koo,Thyroid Disease Awareness Kenya Foundation ,TDAK, Sarah Katulle anaelezea umuhimu wa wagonjwa kuwa kwenye kundi ambapo wanaweza kushirikishana kuhusu mbinu mbadala ya kuishi na matatizo hayo kando na matibabu. Kundi hilo linawasaidia wagonjwa kupata matibabu kwa urahisi kwa kushirikiana na madaktari bingwa ,mahabara maalum na dawa sahihi. Aidha TDAK ili kuwasaidia wagonjwa hao kuishi maisha ya kawaida wakiwa kazini ,inawaandikia barua ambazo zinawasilishwa kwa maajiri kutambua hali halisi ya wagonjwa na mahitaji yao.
-
Mzigo wa uvutaji sigara Misri ulivyo pasua kichwa kwa afya ya wengi
03/06/2025 Duration: 09minMisri ipo kwenye njia panda kuhusu utekelezaji wa sheria zake za kudhibiti matumizi ya tumbaku haswa sigara na Shisha. Kwa njia moja sigara inaleta mapato makubwa kwa mfuko wa mapato ya serikali ya Misri ,ni tabia inayoruhusiwa ila kwa upande mwingine inakodolea macho hatari kubwa ya kiafya inayotokana na uvutaji sigara.Unapowasili Cairo jiji kuu la Misri ,ukutana na harufu tamu ya mikate ,keki na bidhaa zingine za ngano za kuokwa,marashi yanayonukia lakini pia kuna harufu ya shisha, aina ya tumbaku ya kisasa zenye ladhaa za kupendeza lakini pia harufu kali zaidi ya sigara.Zipo sheria zinazokataza uvutaji sigara katika sehemu za umma ,shule ,vituo vya afya ila utekelezaji wake bado ni changamoto kubwa.Kuna mpango pia wa treni mwendo kasi ,maarufu Greenline ambapo uvutaji sigara umeharamishwa.Hata hivyo kibarua bado kipo cha kubadilisha mtazamo wa baadhi ya wananchi wanaoamini uvutaji sigara ni starehe ,kitu cha hadhi na unaweza kufanya hivyo popote muradi usikamatwe.Misri pia inabidi kuangalia kwa jicho
-
Mipango tofauti ya matibabu ya matatizo ya Tezi koo ambayo hutumika Afrika
28/05/2025 Duration: 10minKabla mgonjwa yeyote kuanzishwa kwenye matibabu, awe ana tatizo la tezi koo kuzalisha homoni kupitiliza au kushindwa kuzalisha, ni sharti vipimo maalum kufanyika Kipimo cha kwanzo ni inaangazia homoni tofauti inayozalishwa na tezi koo na hii mtu yeyote anaweza kufanya katika wakati wa kufanya vipimo kujua hali yake ya afya ,hapa mtu si lazima awe ameonesha dalili za tezi koo kuwa na tatizo.Kipimo cha pili ambacho ni muhimu huzingatia zaidi viwango vya homoni tatu muhimu zinazozalishwa na tezi koo ambayo ni (TSH), thyroxine (T4), na triiodothyronine (T3) .Matokeo yataamua ni mpango gani wa matibabu mgonjwa atapewa dawa,kudhibiti homoni au kuzalisha homoni mbadala tezi koo inaposhindza kazi yake.Kando na dawa kama mpango wa matibabu ,wagonjwa wenye uvimbe wanaweza kushauriwa kufanya upasuaji kuondoa tezi koo ,sehemu yake au yote.Kuna pia mpango wa kutumia mianzi na madini ya Iodine maarufu kama Radioiodine mpango ambao ni sharti kufanywa kwa ueledi mkubwa na kwenye vituo vya afya vilivyo na vifaa vya viwa
-
Matatizo ya tezi ya koo ambayo yanaweza kukusababishia matatizo ya akili
20/05/2025 Duration: 10minMatatizo ya tezi ya koo ,kwa kawaida yananaletwa na upungufu au wingi wa madini aina ya iodine ambayo huzalishwa na tezi (thyroid gland). Homoni inapokuwa kidogo hali ambayo inafahamika kama Hypothyroidism, hii inaashiria kwamba tezi inafanya juhudi za hali ya juu kutafuta madini hayo .Mtu aliye na hali hii ,anakuwa hana nguvu ,nywele kudondoka na hata mzunguko wake wa mwezi wa damu huvurugika.Madini hayo yanapokuwa mengi inamanisha tezi inafanya kazi kupitliza kuzalisha homoni iliyozidi kwenye mzunguko wa damu na kuchanganyika na vitu vingene ambavyo husababisha kutengeneza kama sumu fulani ambayo huchoma mafuta yaliyo kwenye hifadhi mwilini, mishipa ya fahamu huathirika kiasi kidogo.Mtu ambaye ameathiriwa na aina hii ya pili, huanza kupunga uzito na umbo la mwili taratibu baadaye madhara yanapoongezeka mtu anaanza kupoteza kumbukumbu, anakuwa na hasira, anakula sana, nywele zinanyonyoka mpaka anapata upara, magoti yanakosa nguvu na mtu anashindwa kutembea.Moyo kwenda mbio , macho yanavimba sehemu ya ju