Habari Rfi-ki

  • Author: Vários
  • Narrator: Vários
  • Publisher: Podcast
  • Duration: 3:56:26
  • More information

Informações:

Synopsis

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episodes

  • Kenya: Vijana wapinga michango ya wanasiasa kanisani

    11/03/2025 Duration: 09min

     Shaba yetu leoinalenga nchini Kenya ambapo Vijana wameanza kuandamana kupinga kile wanadai wanasiasa kutoa kiasi kikubwa cha pesa kwenye maeneo ya kuabudu ili hali wao hawana ajira. Tumekuuliza hatua hii ni sahihi?Haya hapa baadhi ya maoni yako.

  • Kenya : Rais Ruto na mpinzani Raila Odinga kushirikiana

    11/03/2025 Duration: 09min

    Mwishoni mwa juma  lililopita rais wa Kenya William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga walitiliana saini mkataba wa ushirikiano wa kisiasa, wanaosema utasaidia kutatua changamoto  zinazowakabili raia wa taifa hilo.  Unaamini makubaliano ya viongozi hawa ni sahihi?Ndilo swali tumekuuliza na haya hapa maoni yako.

  • Hatua ya rais Donald Trump kusitisha msaada wakijeshi kwa nchi ya Ukraine

    06/03/2025 Duration: 10min
  • Maoni kuhusu vingozi wa kijeshi wa nchi za Afrika Magharibi kutaka kugombea urais

    05/03/2025 Duration: 10min

    Nchini Gabon, kiongozi wa kijeshi jenerali Brice Oligui Nguema ametangaza kuwa atagombea urais katika uchaguzi wa mwezi ujao, baada ya kutwaa madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi ya 2023.Hili linajiri wakati huu viongozi wengine wa kijeshi kwenye nchi za Burkina Faso, Mali na Niger wakielekea kuchukua mkondo huo.

  • Vyama vya upinzani nchini Uganda kufunga kuwaombea wafungwa wa kisiasa

    04/03/2025 Duration: 09min
  • Kila Ijumaa ni mada huru ambapo unatoa maoni kuhusu ulichokiona wiki hii

    28/02/2025 Duration: 10min

    Leo ni Ijumaa ,,siku ya mada huru kwenye habari rafiki  ambapo Tunakupa nafasi ya kuzungumzia suala lolote ambalo limetokea nchini mwako wiki hii au kile ambacho umekisikia kwenye matangazo yetu ya juma hili

  • Rais wa Uganda Yoweri Museveni asikitishwa na hali ya umaskini nchini mwake

    27/02/2025 Duration: 10min

    Mada  ni kuhusu..kauli ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni Akiwa katika ziara ya kawaida kuzungumza na raia wake , ameeleza kuguswa na kusikitishwa na hali ya umasikini anayoshuhudia kwenye nchi yake,,,wakati huu tatizo la umasikini linashuhudiwa pia kwenye mataifa mengine ya ukanda.Tulimuuliza mskilizaji  anazungumziaje kauli ya Rais Museveni na je viongozi wa ukanda wamefanya vyakutosha kupambana na umasikini?

  • Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, atangaza kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa

    24/02/2025 Duration: 10min

    Karibu  kwenye kipindi cha leo ambapo tunaangazia tangazo la  Rais wa DRC, Felix Tschsekedi, kuwa  ataunda Serikali ya umoja wa kitaifa, hatua inayokuja wakati huu akiwa katika shinikizo kutoka ndani na nje ya nchi yake, kuhusu namna alivyoshughulikia mzozo wa mashariki mwa nchi yake, wakati huu waasi wa M23 wakichukua miji zaidi.

  • Mada Huru: Maoni kuhusu habari kuu wiki hii na matukio katika maeneo mbalimbali

    21/02/2025 Duration: 09min

    Ikiwa ni siku ya Ijumaa, ni wakati wa mada huru, yaani tunampatia mskilizaji nafasi kuchangia habari kuu ambazo tumekuwa nazo wiki hii hapa RFI Kiswahili au kutueleza jambo ambalo limetokea nchini mwake juma hili. Leo pia msikilizaji ni siku ya lugha mama, ningependa sana nikusalimie kwa lugha yako mama lakini ningependa kusikia kutoka kwako kwanza. Jambo! 

  • Maoni: Marekani yaanza mazungumzo na Urusi ya kusitisha vita nchini Ukraine.

    21/02/2025 Duration: 09min

    Haya ni makala ya Habari Rafiki tukiangazia maoni ya waskilizaji wa RFI Kiswahili kuhusu mada kwamba, Marekani imeanza mazungumzo na Urusi, lengo likiwa kupata mkataba wa kusitisha vita nchini Ukraine. Ukraine ambayo haijashirikishwa kwenye mchakato huo inasema haitakubali mkataba wowote bila kuhusishwa.Tumemuuliza msikilizaji je, Marekani inaweza kumaliza vita vya Ukraine? Na anafikiri ni kwanini Marekani haijaishirikisha Ukraine na mataifa ya Ulaya kwenye harakati hizi?

  • Wanamgambo wa RSF waandaa mkutano wa kuunda serikali mbadala Nairobi

    19/02/2025 Duration: 10min

    Wanamgambo wa RSF wanaopigana na jeshi nchini Sudan na washirika wake wakiwemo wanasiasa wapo jijini Nairobi nchini Kenya, wanakojadiliana kuhusu uundwaji wa serikali mbadala wakati huu inapoendelea na vita.Unazungumzia vipi harakati hizi za RSF ?Unafikiri ni kwanini Kenya imewaruhusu wanamgambo hao kukutana katika nchi yake ?

  • Kikao cha usalama wa DRC na Sudan chakamilika Ethiopia bila suluhu

    17/02/2025 Duration: 10min

    Makala ya leo yanaangazia Kikao cha viongozi wa Afrika, kilichotamatika rasmi mwishoni mwa juma lililopita nchini Ethiopia, mzozo wa DRC na Sudan ukigubika mijadala yao.Hata hivyo vikao hivyo  vimekamilika  bila suluhu ya mizozo ya nchi zote mbili, ambapo vyongozi  waliishia kwa kutoa wito wa kusitisha mapigano. tulimuuliza msikilizaji iwapo anaridhika na matokeo ya kikao hicho na  anadhani nini cha zaidi viongozi hawa wangefanya kukomesha mizozo barani Afrika

  • Mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Afrika kuzingatia usalama wa DRC

    13/02/2025 Duration: 10min

    Mkutano wa kila mwaka wa viongozi wa Afrika umeanza rasmi jijini Addis Ababa, #Ethiopia ambapo maswala muhimu ikiwemo usalama mashariki mwa #DRC, mapinduzi ya kijeshi na vita dhidi ya makundi ya kijihadi yakitarajiwa kugubika mkutano huu.Tulimuuliza mskilizaji natarajia nini kipya kutoka kwa viongozi wa AU? na iwapo anafikiri viongozi wameshindwa kumaliza changamoto za bara hili..

  • Kauli ya rais Donald Trump kuhamisha wapalestina yapingwa vikali

    12/02/2025 Duration: 10min

    Kwenye kipindi cha leo tunaangazia kauli  tata ya Rais Donald #trump, kuhusu mzozo wa #Gaza, safari hii akitishia kuvunjika kwa mkataba wa usitishaji mapigano, ikiwa Hamas haitawaachia mateka wote ifikapo Jumamosi ya wiki hii.Juma lililopita alidai kuwa nchi yake itachukua udhibiti wa Gaza na kuwahamisha Wapalestina.Tulimuuliza mskilizaji anazungumziaje kauli hiyo ya Trump and je huenda zikachochea mzozo zaidi kati ya #Israel na Hamas?

  • Hatua ya Kenya kuondoa mahojiano kwa waomba vitambulisho yaibua hisia mseto

    11/02/2025 Duration: 09min

    Makala haya yanaangazia hatua ya Serikali ya kenya  kusema  hakutakuwa na haja ya mahojiano kwa waomba vitambulisho toka katika maeneo ya mpakani, uamuzi ambao umeibua mjadala kuhusu masuala ya usalama.Tulimuuliza msikilizaji anazungumziaje hatua hiyo ya Kenya  vile vile nchini mwake hali ikoje

  • Kauli ya mkutano wa SADC na EAC kuhusu amani nchini DRC waibua maoni mseto

    10/02/2025 Duration: 09min

     kwenye makala ya leo tunaangazia  hatua ya  wakuu wa nchi za #SADC na EAC kutaka kusitishwa mapigano maramoja ,na kutaka  kuondoka kwa vikosi vya kigeni mashariki mwa #DRC, pamoja na Serikali ya Kinshasa kuzungumza moja kwa moja na waasi wa #M23 ambapo  wito huo  umepokelewa kwa hisia mseto na raia wa ukanda.

  • Kila siku ya Ijumaa huwa tunaangazia mada huru kwenye makala habari rafiki

    31/01/2025 Duration: 10min

    Kila siku ya  ijumaa ni mada huru  ambapo Tunampa nafasi  msikilizaji kujadili suala lolote ambalo limetokea nchini mwake wiki hii au kile ambacho amekisikiliza kwenye habari zetu juma hili.

  • Changamoto za upatikanaji wa Nishati ya Uhakika barani Afrika

    30/01/2025 Duration: 09min

    Wakuu wa nchi za Afrika walikutana juma hili nchini Tanzania ambapo walijadiliana kuhusu changamoto za upatikanaji wa Nishati ya Uhakika katika mataifa hayo.Licha ya rasilimali za bara la Afrika bado hakuna nishati ya uhakika na endelevu? Bonyeza uskilize maoni mbalimbali.

  • Athari za Donald Trump kusitisha misaada kwa Afrika na njia mbadala kujitegemea

    30/01/2025 Duration: 10min

    Uamuzi wa Rais wa Marekani #DonaldTrump, kuagiza kusitishwa kwa muda utowaji wa misaada yote ya kigeni umeibua mjadala na sintofahamu hasa kwa nchi za Afrika, ambazo sekta muhimu ikiwemo afya zinategemea msaada wa Marekani.Tulimuuliwa msikilizaji anazungumziaje hatua hii ya Marekani na Nchi za Afrika zifanye nini kuacha kutegemea misaada ya nchi za Kigeni?

  • Swali: Je viongozi wa Afrika wanaweza kutatua migogoro inayokumba bara hilo

    29/01/2025 Duration: 09min

    Mizozo inayosibu ukanda wa Afrika ya Mashariki inaendelea kuongezeka, ikiwemo Sudan Kusini na sasa DRC. Viongozi wa Afrika wanasisitiza matatizo ya Afrika sharti kutatuliwa kwa suluhu kutoka Afrika. Je hili linawezekana?

page 1 from 2