Synopsis
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Episodes
-
Nosizi Ndube: Kukosa utaifa haikukwamisha ndoto yangu ya elimu, asante UNHCR na wadau mbalimbali
09/01/2025 Duration: 05minShirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 ni wa kwanza katika jamii ya Washona wanaoishi mjini Nairobi Kenya kupata elimu katika ngazi hiyo. Mpango wa UNHCR wa kupambana na kutokuwa na utaifa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya umekuwa chachu ya mafanikio ya msichana huyo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya alimtembelea Nosizi nyumbani kwake ili kupata undani wa safari yake..
-
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "Kwego"
09/01/2025 Duration: 01minKatika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KWEGO"
-
09 JANUARI 2025
09/01/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina inayotupeleka Kenya ambapo Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchaambizi wa neno KWEGO.Mwezi mmoja tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar Al-Assad, zaidi ya wakimbizi 125,000 wamerejea Syria "wakiwa na matumaini baada ya miaka mingi ya kuishi uhamishoni", lakini wamejikuta wakikabiliwa na hali mbaya nchini mwao, wameeleza leo wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Likiwa linaongoza wito kwa jumuiya ya kimataifa "kutoka kwenye maneno hadi vitendo" ili kuwasaidia watu walio waliorejea ambao sasa wako katika mazingira magumu, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limesema familia nyingi zina uhaba wa makazi na njia kidogo za kiuchumi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeongeza ombi lake la fedha kufikia dola milioni 73.2 kwa ajili ya kusa
-
UNICEF Burundi: Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii
08/01/2025 Duration: 03minShirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Burundi katika kuunganisha taarifa za watu katika mifumo inayosomana ya kiraia na ya huduma ya afya. Euphrasie Butoyi mama akiwa amembeba mtoto wake mchanga, amekuja katika ofisi za msajili za eneo la Busoni jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, anasema,“kabla ilikuwa vigumu kumwandikisha mtoto. Umbali ulikuwa mrefu. Tulikuwa tunalazimika kulipia tiketi ya safari kwa ajili yetu na mashahidi. Tulikuwa tunaweza kwenda kule hata mara mbili bila kupata cheti cha kuzaliwa.” Damien Ndayisenga ni msajili wa kijamii anathibitisha hilo kwa kusema, “ukweli kabla ya hatua hii, ofisi ya usajili wa raia ya Busoni ilikuwa imezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaokuja kusajili watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa. Lakini huduma hii imerahisisha.” Hakika mradi huu umekuwa mkombozi kama anavyoendelea kueleza Euphrasie Butoyi. Anaposema faranga elfu 10 fedha ya Burundi hiyo ni takribani dola nne za kimarekani, “leo tofauti ni kuwa k
-
Msichana Bangladesh: Sikufahamu ufundi bomba ni nini, sasa ILO imeniwezesha
08/01/2025 Duration: 01minNchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.Video ya ILO hapa Cox’s Bazaar inamleta kwako mmoja wa wanufaika hao ambaye hata hivyo jina lake halikutajwa, akiwa ameshikilia vifaa vya ufundi bomba anasema, awali sikufahamu kuhusu hii kozi hadi nilipofahamu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana. Hii ni mara ya kwanza fursa hii imetufikia katika shule ya sekondari ya juu ya Moheshkhali. Tunajifunza stadi badala ya kupoteza muda nyumbani itanisaidia maisha yangu ya baadaye.Nikihitimu masomo naungana na kaka kwenye duka lakeAnakiri kuwa kabla ya kushiriki mafunzo haya hakuwa anafahamu kabisa ufundi bomba ni kitu gani. Lakini sasa amejifunza
-
Gaza: Zaidi ya watoto 70 wameuawa tangu Januari 1 huku gharama za maisha zikizidi kupanda
08/01/2025 Duration: 01minHali ya maisha kwa raia wa Gaza inaendelea kuwa mbaya msimu huu wa baridi kali kutokana na vikwazo vya kufikisha misaada, kupanda kwa gharama za maisha na mashambuizi yanayoendelea kukatili maisha ya raia wakiwemo watoto 74 waliouawa tangu Januri Mosi mwaka huu yamesema mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema kuuawa kwa watoto hao 74 katika siku saba za kwanza za mwezi huu ni dhihirisho la jinamizi linaloendelea kuighubika Gaza na mashambulizi ya Israel hayaonyeshi dalili yoyote ya kukoma ikiwemo ya jana usiku katika mji wa Gaza, Khan Younis na kwenye makazi ya Pwani ya wakimbizi wa ndani ya Al Mawasi ambayo Israel yenyewe iliyatenga hapo awali kama maeneo salama. Kwa mujibu wa UNICEF jana Jumanne pekee watoto 5 wameripotiwa kuuawa Al Mawasi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEFF Catherine Russell amesema "Kwa watoto wa Gaza, mwaka mpya umeleta vifo zaidi na mateso kutokana na mashambulizi, kunyimwa huduma, na kuongezeka kwa hali y
-
08 JANUARI 2025
08/01/2025 Duration: 09minZaidi ya watoto 70 wameuawa Gaza tangu Januari 1 huku gharama za maisha zikizidi kupanda.Mafunzo ya ufundi bomba kuniwezesha kutunza familia yangu – Msichana Bangladesh.Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii Burundi.Mashinani nchini Tanzania kuhusu haki za watoto
-
07 JANUARI 2025
07/01/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo kushuhudia jinsi Umoja wa Mataifa unavyowasaidia wanawake waathrika wa ukatili wa kingoni kuweza kujitegemea na kumudu mahitaji ya familia zao.Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, takriban watu 5,601 waliuawa nchini Haiti mwaka 2024 kutokana na ghasia za magenge, likiwa ni ongezeko la zaidi ya mauaji 1,000 ya mwaka 2023. Katika moja ya matukio mabaya zaidi na ya kushtua mwaka jana, takriban watu 207 waliuawa mapema Desemba kwenye mauaji yaliyoratibiwa na kiongozi wa genge lenye nguvu la Wharf Jérémie katika eneo la Cité Soleil huko Port-au-Prince. Wengi wa waliouawa walikuwa wazee walioshutumiwa kusababisha kifo cha mtoto wa kiongozi huyo kwa njia ya uchawi.Leo, Umoja wa Mataifa na Serikali ya Lebanon wametoa ombi la nyongeza ya dola milioni 371.4 za kimarekani, zikilenga kutoa msaada wa kuokoa maisha ya walioathiriwa na mzozo wa hivi karibuni
-
Raia wa Mali walioko ughaibuni waonesha mfano bora wa kuwekeza nyumbani
06/01/2025 Duration: 03minMfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa kushirikiana na wadau na kupitia msaada wa Muungano wa Ulaya unasaidia raia wa Mali wanaoishi ughaibuni kuwekeza kwa ufanisi nyumbani Mali.Wamefanya hivyo kwa kuwasaidia kuanzisha Ciwara Capital, kampuni ya uwekezaji inayomilikiwa na raia wa Mali na sasa wanasaidia wakulima wa mpunga nchini Mali kuimarisha na kuongeza uzalishaji wa mpunga, ikiwemo eneo la Mopti ambalo limekuwa likikabiliwa na ukosefu wa usalama na hivyo wakulima kugubikwa na umaskini.Mfumo huu unadhihirisha kuwa badala ya waafrika kutuma dola bilioni 55 kila mwaka nyumbani kusaidia familia, fedha hizo zinaweza kuwekezwa kwenye miradi endelevu. Je ni kwa vipi, Assumpta Massoi anafafanua kwenye makala hii iliyoandaliwa na IFAD.
-
Kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya ni muhimu kama ilivyo kujiandaa - Ugonjwa wa HMPV
06/01/2025 Duration: 02minHuku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
-
06 JANUARI 2025
06/01/2025 Duration: 09minHii leo jaridani tunaangazia magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus, na watoto waathirika wa vita Gaza. Makala inatupeleka nchini Mali na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi.Baada ya miezi 14 ya vita Gaza maelfu ya watu wakiwemo watoto wamesalia na ulemavu wa maisha kwa kulazimika kukatwa viungo kutokana na kujeruhiwa katika vita inayoendelea kwa miezi 15 akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 Mahmmoud ambaye sasa amepooza baada ya kupigwa risasi mgongon
-
Mzazi wa Mahmooud: Mwanangu amepata kilema cha maisha sababu ya vita isiyokoma Gaza
06/01/2025 Duration: 02minBaada ya miezi 14 ya vita Gaza maelfu ya watu wakiwemo watoto wamesalia na ulemavu wa maisha kwa kulazimika kukatwa viungo kutokana na kujeruhiwa katika vita inayoendelea kwa miezi 15 akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 Mahmmoud ambaye sasa amepooza baada ya kupigwa risasi mgongoni na anahitaji huduma za haraka za afya ili akatibiwe limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. Taarifa ya Thelma Mwadzaya inafafanua zaidi
-
Faida ya magari ya umeme inaweza isionekane kwa sasa lakini si muda mrefu yatakuwa na manufaa kwa mazingira na uchumi
03/01/2025 Duration: 03minKijana Mtanzania Gibson Kawago hivi karibuni kupitia kampuni yake ya WAGA inayoshughulika na uvumbuzi wa teknolojia zinazolenga kupambana na uchafuzi wa mazingira ya ulimwengu, ametangaza kuanzisha vifaa vinavyotumika kuchaji magari ya umeme lengo likiwa ni kuwasaidia watu wa eneo lake, Afrika Mashariki kupata huduma ya kuchaji magari yao ili wahame kutoka katika matumizi ya mafuta ya kisukuku kama petroli na dizeli. Lakini je ana majibu gani kwa wale ambao bado hawaoni faida ya ya magari ya umeme kwa mazingira ikiwa bado vyanzo vya umeme ni chafuzi? Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Gibson anafafanua.
-
UN: Vifo vitokanavyo na baridi Gaza vinazuilika, usitishaji mapigano na misaada ndio jawabu
03/01/2025 Duration: 01minShirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeonya juu ya vifo vitokanavyo na msimu wa baridi kali Gaza likisema limesikitishwa sana na athari mbaya za mvua za msimu wa baridi na baridi kali kwa Wapalestina waliokimbia makazi yao na kuishi katika mazingira magumu huko Gaza, kwani hilo ni janga la kibinadamu lisilo na kifani. Kupitia taarifa iliyotolewaleo mjini Geneva Uswisi Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope amesema "Watu walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na takriban watoto wachanga saba, wamekufa kutokana na baridi kali au hypothermia, na vifo hivi vya kusikitisha vinasisitiza haja ya haraka ya makazi na msaada mwingine wa kibinadamu kuwafikia watu wa Gaza mara moja," Ameongeza kuwa hali hii inachochea janga zaidi la kibinadamu ambalo tayari linawakumba watu waUkanda wa Gaza. Mvua kubwa na mafuriko yameyakumba makazi ya wakimbizi wa ndani yaliyojengwa kwa mahema na kulazimisha familia kuachwa katika maeneo ya wazi kwenye hali mbaya ya baridi, zikijitahidi kutengeneza mah
-
Papua New Guinea: Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake zapatiwa ‘muarobaini’
03/01/2025 Duration: 02minKila mwaka, mamia ya wanawake nchini Papua New Guinea, taifa la visiwani katika bahari ya Pasifiki, hushutumiwa kimakosa kuwa ni wachawi. Matokeo yake hukumbwa na ukatili miongoni mwa wanajamii. Hata hivyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP nchini humo, limechukua hatua.Kiongozi mkubwa wa Kijiji chetu alifariki dunia, na tulipoenda kwenye maziko, ambapo kila mtu alisema sisi ni wachawi na tulikula moyo wake. Ni kauli ya Annabele, jina lake halisi limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake akielezea tuhuma zilizowakabili kwenye jamii yao ya jimbo la Enga nchini Papua New Guinea, hadi kushambuliwa kwa nondo za moto na nyumba zao kuteketezwa kwa moto. Video ya UNDP inamnukuu akisema kuwa walikuwa 9, ambapo wanne walifariki dunia na watano akiwemo Annabele, walinusurika, “kesho yake asubuhi Askofu na wenzake walifika, halikadhalika jeshi na polisi, na ndio walituokoa.” Askofu huyo Justine Soongie Dayosisi ya Wabag jimboni Enga anasema walipowachukua waliambiwa wahaki
-
03 JANUARI 2025
03/01/2025 Duration: 09minVifo vitokanavyo na baridi Gaza vinazuilika, usitishaji mapigano na misaada ndio jawabu: UN.Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake Papua New Guinea zapatiwa ‘muarobaini’ na UNDP.Makala ni kuhusu Gibson Kawago, mwanzilishi wa kampuni ya WAGA akizungumzia kuanzisha vifaa vya kuchaji magari ya umeme Tanzania.Mashinani ni IFAD Zimbabwe.
-
31 DESEMBA 2024
31/12/2024 Duration: 12minKipindi maalumu wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wenyeji wao wanaeleza namna walivyonufaika na misaada ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake na pia wanaeleza matumaini yao kwa mwaka ujao wa 2025.
-
-
-
30 DESEMBA 2024
30/12/2024 Duration: 10minLeo jaridani: Mwaka 2024 ulighubikwa na machungu lakini kuna matumaini 2025 asema Guterres.UNMAS yaondolea hofu wakulima Beni, DRC kwa kutegua masalia ya mabomu.Makala inatupeleka Uganda kusikiliza msichana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Ashiimwe Baganiza mwenye ndoto ya kuwa wakili ili kuwatetea wanawake.Mashinani ni mradi wa Siku 1000 wa UNICEF Zambia.