Habari Za Un

31 JANUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tutakuletea simulizi ya wakimbizi wa ndani nchini humo. Makala inatupeleka nchini Senegal na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni?Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia..Kutana na mkimbizi Masimango Mango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambaye kwa sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagara Goma jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC, anasema kwa hakika vita imemchosha na anacholilia ni amani ili arejee nyumbani na familiia yake.Makala tunakwenda Senegal, magharibi mwa AFrika ambako nishati ya umeme imeleta mabadiliko makubwa kwenye kijiji ambacho awali kiligubikwa na kiza nyakati za usiku.Na katika Zulaikha kutoka Afghanistan ambaye ana matumaini katika msimu huu wa baridi kutokana na msaada wa fedha kutoka Shirika la Marekani