Habari Za Un

Hali ni tete mashariki mwa DRC, msaada wa kibinadamu haufikii wahitaji - Mashirika

Informações:

Synopsis

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia. Selina Jerobon amefuatilia matamko ya mashirika hayo na kutuandalia taarifa ifuatayo. Janga la haki za binadamu katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) linaendelea kuzidi kuwa baya kutokana na ripoti zinazonyesha kuwa kundi la wapiganaji la M23 limeendelea kusonga kusini kuelekea Bukavu, imeeleza Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) leo Januari 31 mjini Geneva, Uswisi.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) katika taarifa iliyotolewa katika mji Mkuu wa DRC, Kinshasa, limesema licha ya juhudi hizo zinazoendelea ili kusaidia watu, kuongezeka kwa ghasia kumelazimisha IOM na mashirika mengine ya kibinadamu kusitisha operesheni katika maeneo yaliyoathirika zaidi, na hivyo kusitisha msaada wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu.Kwa upande wak