Habari Za Un

03 FEBRUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC, na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na mashinani tunarejea DRC, kulikoni?Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi.Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani.Makala inatupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwenye kambi ya wakimbizi ya Korsi inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 kut