Habari Za Un

06 FEBRUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwakina inayotupeleka Havan Cuba ambapo mmoja wa walumbi wa lugha ya Kiswahili Jorum Nkumbi, ambaye pia ni mwandishi wa vitabu anayetumia sanaa ya uandishi wa vitabu kuitangaza lugha mama yake ya Kiswahili amezindua kitabu kipya hivi karibuni wakati wa kongamano la kimataifa la Kiswahili. Mengine tuliyokuandalia ni kama yafuatayo.Yerusalem Mashariki eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli ambako Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Tom Fletcher yuko ziarani na amepata shuhuda halisi za wanaokabiliwa na kufurushwa makwao. Mmoja wao ni Um Nasser ar Rajabi ambaye amemweleza kuwa Nimekuwa kwenye ndoa katika nyumba hii kwa miaka 50.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu mahitaji ya dharura ya ulinzi na mazingira magumu yanayokabili raia kwenye eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC lenye utajiri mkubwa wa madini, wakati huu uhasama ulioshika kasi tangu mwezi uliopita kati ya jeshi la serikali n