Habari Za Un

30 JANUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea mad akwa kina inayotupeleka nchini Tanzania ambapo Chuo cha ulinzi wa amani kwa kushirikiana na wataalamu kutoka ‘UNITA’ na Idara ya Umoja wa Mataifa ya Operesheni za Ulinzi waliandaa mpango wa ufundishaji kuhusu ulinzi wa amani, Brigedia Jenerali George Itang’are ambaye Mkuu wa chuo hicho anaelezaIkiwa leo ndio siku ambayo Israeli ilitaka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA liwe limefunga shughuli zake Ukanda wa Gaza, Msemaji wa UNRWA Julie Touma amenukuliwa akisema hadi sasa hawajapokea mawasiliano yoyote rasmi ya jinsi ya kutekeleza sheria ya Bunge la Israeli, Knesset inayotaka waondoke.Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi wa dharura, CERF umetenga dola milioni 17 kufanikisha operesheni za kiutu nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mapigano makali huko Kivu kaskazini na Kivu Kusini yameacha mamia ya maelfu ya wakimbizi wakiwa na mahitaji makubwa ya kibinadamu.Na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, jana Januari 29 w