Habari Za Un
Papua New Guinea: Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake zapatiwa ‘muarobaini’
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:02:08
- More information
Informações:
Synopsis
Kila mwaka, mamia ya wanawake nchini Papua New Guinea, taifa la visiwani katika bahari ya Pasifiki, hushutumiwa kimakosa kuwa ni wachawi. Matokeo yake hukumbwa na ukatili miongoni mwa wanajamii. Hata hivyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP nchini humo, limechukua hatua.Kiongozi mkubwa wa Kijiji chetu alifariki dunia, na tulipoenda kwenye maziko, ambapo kila mtu alisema sisi ni wachawi na tulikula moyo wake. Ni kauli ya Annabele, jina lake halisi limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake akielezea tuhuma zilizowakabili kwenye jamii yao ya jimbo la Enga nchini Papua New Guinea, hadi kushambuliwa kwa nondo za moto na nyumba zao kuteketezwa kwa moto. Video ya UNDP inamnukuu akisema kuwa walikuwa 9, ambapo wanne walifariki dunia na watano akiwemo Annabele, walinusurika, “kesho yake asubuhi Askofu na wenzake walifika, halikadhalika jeshi na polisi, na ndio walituokoa.” Askofu huyo Justine Soongie Dayosisi ya Wabag jimboni Enga anasema walipowachukua waliambiwa wahaki