Habari Za Un

UN: Vifo vitokanavyo na baridi Gaza vinazuilika, usitishaji mapigano na misaada ndio jawabu

Informações:

Synopsis

Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeonya juu ya vifo vitokanavyo na msimu wa baridi kali Gaza likisema limesikitishwa sana na athari mbaya za mvua za msimu wa baridi na baridi kali kwa Wapalestina waliokimbia makazi yao na kuishi katika mazingira magumu huko Gaza, kwani hilo ni janga la kibinadamu lisilo na kifani. Kupitia taarifa iliyotolewaleo mjini Geneva Uswisi Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope  amesema "Watu walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na takriban watoto wachanga saba, wamekufa kutokana na baridi kali au hypothermia, na vifo hivi vya kusikitisha vinasisitiza haja ya haraka ya makazi na msaada mwingine wa kibinadamu kuwafikia watu wa Gaza mara moja," Ameongeza kuwa hali hii inachochea janga zaidi la kibinadamu ambalo tayari linawakumba watu waUkanda wa Gaza. Mvua kubwa na mafuriko yameyakumba makazi ya wakimbizi wa ndani yaliyojengwa kwa mahema na kulazimisha familia kuachwa katika maeneo ya wazi kwenye hali mbaya ya baridi, zikijitahidi kutengeneza mah