Habari Za Un

06 JANUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunaangazia magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus, na watoto waathirika wa vita Gaza. Makala inatupeleka nchini Mali na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi.Baada ya miezi 14 ya vita Gaza maelfu ya watu wakiwemo watoto wamesalia na ulemavu wa maisha kwa kulazimika kukatwa viungo kutokana na kujeruhiwa katika vita inayoendelea kwa miezi 15 akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 Mahmmoud ambaye sasa amepooza baada ya kupigwa risasi mgongon