Habari Za Un
07 JANUARI 2025
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:09:58
- More information
Informações:
Synopsis
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo kushuhudia jinsi Umoja wa Mataifa unavyowasaidia wanawake waathrika wa ukatili wa kingoni kuweza kujitegemea na kumudu mahitaji ya familia zao.Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, takriban watu 5,601 waliuawa nchini Haiti mwaka 2024 kutokana na ghasia za magenge, likiwa ni ongezeko la zaidi ya mauaji 1,000 ya mwaka 2023. Katika moja ya matukio mabaya zaidi na ya kushtua mwaka jana, takriban watu 207 waliuawa mapema Desemba kwenye mauaji yaliyoratibiwa na kiongozi wa genge lenye nguvu la Wharf Jérémie katika eneo la Cité Soleil huko Port-au-Prince. Wengi wa waliouawa walikuwa wazee walioshutumiwa kusababisha kifo cha mtoto wa kiongozi huyo kwa njia ya uchawi.Leo, Umoja wa Mataifa na Serikali ya Lebanon wametoa ombi la nyongeza ya dola milioni 371.4 za kimarekani, zikilenga kutoa msaada wa kuokoa maisha ya walioathiriwa na mzozo wa hivi karibuni