Habari Za Un
Gaza: Zaidi ya watoto 70 wameuawa tangu Januari 1 huku gharama za maisha zikizidi kupanda
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:01:55
- More information
Informações:
Synopsis
Hali ya maisha kwa raia wa Gaza inaendelea kuwa mbaya msimu huu wa baridi kali kutokana na vikwazo vya kufikisha misaada, kupanda kwa gharama za maisha na mashambuizi yanayoendelea kukatili maisha ya raia wakiwemo watoto 74 waliouawa tangu Januri Mosi mwaka huu yamesema mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema kuuawa kwa watoto hao 74 katika siku saba za kwanza za mwezi huu ni dhihirisho la jinamizi linaloendelea kuighubika Gaza na mashambulizi ya Israel hayaonyeshi dalili yoyote ya kukoma ikiwemo ya jana usiku katika mji wa Gaza, Khan Younis na kwenye makazi ya Pwani ya wakimbizi wa ndani ya Al Mawasi ambayo Israel yenyewe iliyatenga hapo awali kama maeneo salama. Kwa mujibu wa UNICEF jana Jumanne pekee watoto 5 wameripotiwa kuuawa Al Mawasi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEFF Catherine Russell amesema "Kwa watoto wa Gaza, mwaka mpya umeleta vifo zaidi na mateso kutokana na mashambulizi, kunyimwa huduma, na kuongezeka kwa hali y