Habari Za Un
Msichana Bangladesh: Sikufahamu ufundi bomba ni nini, sasa ILO imeniwezesha
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:01:40
- More information
Informações:
Synopsis
Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.Video ya ILO hapa Cox’s Bazaar inamleta kwako mmoja wa wanufaika hao ambaye hata hivyo jina lake halikutajwa, akiwa ameshikilia vifaa vya ufundi bomba anasema, awali sikufahamu kuhusu hii kozi hadi nilipofahamu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana. Hii ni mara ya kwanza fursa hii imetufikia katika shule ya sekondari ya juu ya Moheshkhali. Tunajifunza stadi badala ya kupoteza muda nyumbani itanisaidia maisha yangu ya baadaye.Nikihitimu masomo naungana na kaka kwenye duka lakeAnakiri kuwa kabla ya kushiriki mafunzo haya hakuwa anafahamu kabisa ufundi bomba ni kitu gani. Lakini sasa amejifunza