Habari Za Un
UNICEF Burundi: Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii
- Author: Vários
- Narrator: Vários
- Publisher: Podcast
- Duration: 0:03:29
- More information
Informações:
Synopsis
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Burundi katika kuunganisha taarifa za watu katika mifumo inayosomana ya kiraia na ya huduma ya afya. Euphrasie Butoyi mama akiwa amembeba mtoto wake mchanga, amekuja katika ofisi za msajili za eneo la Busoni jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, anasema,“kabla ilikuwa vigumu kumwandikisha mtoto. Umbali ulikuwa mrefu. Tulikuwa tunalazimika kulipia tiketi ya safari kwa ajili yetu na mashahidi. Tulikuwa tunaweza kwenda kule hata mara mbili bila kupata cheti cha kuzaliwa.” Damien Ndayisenga ni msajili wa kijamii anathibitisha hilo kwa kusema, “ukweli kabla ya hatua hii, ofisi ya usajili wa raia ya Busoni ilikuwa imezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaokuja kusajili watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa. Lakini huduma hii imerahisisha.” Hakika mradi huu umekuwa mkombozi kama anavyoendelea kueleza Euphrasie Butoyi. Anaposema faranga elfu 10 fedha ya Burundi hiyo ni takribani dola nne za kimarekani, “leo tofauti ni kuwa k