Habari Za Un

09 JANUARI 2025

Informações:

Synopsis

Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina inayotupeleka Kenya ambapo Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchaambizi wa neno KWEGO.Mwezi mmoja tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar Al-Assad, zaidi ya wakimbizi 125,000 wamerejea Syria "wakiwa na matumaini baada ya miaka mingi ya kuishi uhamishoni", lakini wamejikuta wakikabiliwa na hali mbaya nchini mwao, wameeleza leo wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Likiwa linaongoza wito kwa jumuiya ya kimataifa "kutoka kwenye maneno hadi vitendo" ili kuwasaidia watu walio waliorejea ambao sasa wako katika mazingira magumu, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limesema familia nyingi zina uhaba wa makazi na njia kidogo za kiuchumi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeongeza ombi lake la fedha kufikia dola milioni 73.2 kwa ajili ya kusa