Habari Za Un

Nosizi Ndube: Kukosa utaifa haikukwamisha ndoto yangu ya elimu, asante UNHCR na wadau mbalimbali

Informações:

Synopsis

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 ni wa kwanza katika jamii ya Washona wanaoishi mjini Nairobi Kenya kupata elimu katika ngazi hiyo. Mpango wa UNHCR wa kupambana na kutokuwa na utaifa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya umekuwa chachu ya mafanikio ya msichana huyo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya alimtembelea Nosizi nyumbani kwake ili kupata undani wa safari yake..