Synopsis
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
Episodes
-
Changamoto na fursa kwa vijana wajasiriamali na ajira kwenye nchi za Afrika Mashariki
15/05/2024 Duration: 09minHujambo msikilizaji wa rfikiswahili popote pale unapotegea sikio matangazo yetu nikukaribishe katika makala ya Gurudumu la Uchumi, na hivi leo tunaangazia ukanda wa Afrika Mashariki, eneo lililojaa nguvu kazi ya vijana pamoja na ari ya ujasiriamali, lakini bado linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa ajira. Takwimu za hivi karibuni za benki ya dunia zinaonesha uhalisia wa tatizo, takwimu zikitofautiana baina ya nchi na nchi, lakini kiujumla ni kuanzia kati ya asilimia 4 hadi 19 ya vijana hawana ajira, huku wanawake walioko vijijini wakiwa waathirika wakubwa. Katika makala haya hivi leo, tutaangazia kwa kina namna gani bora ya kukabiliana na tatizo la ajira na kuongeza wajasiriamali wengi zaidi kwenye ukanda. Kwenye line ya simu nimewaalika, Ali Mkimo, yeye ni mchambuzi wa masuala ya Uchumi pamoja na Emmanuel Cosmas, kijana mbunifu wa masuala teknolojia na nibalozi wa UNICEF, wote hawa wakiwa nchini Tanzania.
-
Mchango wa biashara ndogondogo na kati kwa uchumi wa nchi za Afrika Mashariki
10/05/2024 Duration: 08minMakala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia mchango na changamoto ya biashara ndogondogo na zile za kati kwenye nchi za Afrika Mashariki.Matayarishaji amezungumza na wafanyabiashara wadogowadogo na kati nchini Kenya, lakini mchambuzi wa masuala ya uchumi Ally Mkimo.
-
Afrika na madai ya mabadiliko katika mifumo ya kifedha ya kimataifa
01/05/2024 Duration: 09minMsikilizaji katika miaka ya hivi karibuni, wito umeendelea kutolewa na mataifa ya Afrika kuhusu kuwepo usawa na haki katika mfumo wa kifedha duniani, ambao Kihistoria, nchi za Kiafrika zimekuwa katika hali mbaya linapokuja suala la kupata ufadhili, rasilimali, na makubaliano yenye usawa ya kibiashara.Kuzungumzia hili, nimemualika kwa njia ya simu kutoka Tanzania, Walter Nguma, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara.
-
Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu
11/04/2024 Duration: 10minKulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii.