Synopsis
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Episodes
-
Kenya: Nani atatamba kwenye "Debi ya Mashemeji" AFC Leopards vs Gor Mahia?
29/03/2025 Duration: 23minMiongoni tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya raga mkondo wa HongKong 7s, sakata la upangaji mchezaji dhidi ya golikipa wa Kenya Patrick Matasi, maandalizi ya debi ya Mashemeji, Misri yapewa haki za kuandaa AFCON U20 huku CAF ikiifungulia uwanja wa Benjamin Mkapa, tuzo nono kwa washindi wa Kombe la Dunia la vilabu, kocha wa Brazil atimuliwa naye Djokovic akikaribia kushinda taji lake la 100.
-
Mashindano ya kukimbiza magari, yapamba moto nchini Kenya
22/03/2025 Duration: 23minMashindano ya dunia ya kukimbiza magari, Safari Rally yanaendelea nchini Kenya. Madereva mbalimbali kutoka duniani, wanakutana mjini Naivasha kwa ajili ya kutafuta ubingwa wa mwaka 2025.
-
CAF: Motsepe achanguliwa tena kuwa rais kwa muhula wa pili wa miaka minne
15/03/2025 Duration: 23minTuliyokuandalia Jumamosi hii ni pamoja na uchaguzi wa CAF, uwanja wa Mkapa wafungiwa kwa muda, michuano ya kufuzu dimba la dunia kwa kina dada chini ya umri wa miaka 17, maandalizi ya mashindano ya kuendesha magari ya WRC Safari Rally, uchambuzi wa mechi za klabu bingwa Ulaya hatua ya kumi na sita bora naye Neymar alazimika kuaga kikosi cha Brazil kufuatia jeraha
-
Misri, Morocco,Tunisia zang'ara mashindano ya tenisi ya vijana chini ya miaka 14
02/03/2025 Duration: 23minTuliyokuandalia hii leo ni pâmoja na matokeo ya mashindano ya tenisi ya vijana barani Afrika chini ya miaka 14, kocha mpya wa Kenya ni nani, matokeo ya mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, timu sita kushiriki ligi ya Afrika ya basketboli kwa mara ya kwanza, huku Afrika Kusini ikijiandaa kutuma ombi rasmi la kuandaa mkondo mmoja wa F1 na Jose Mourinho apata afueni baada ya adhabu yake kupunguzwa.