Synopsis
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
Episodes
-
Nani ataisadia Sudan Kusini, isirejee kwenye vita ?
19/03/2025 Duration: 10minSudan Kusini inakabiliwa na wasiwasi wa kujipata tena kwenye vita vipya, kufuatia mzozo wa hivi punde kati ya vikosi vya rais Salva Kiir na Makamu wake wa kwanza wa Riek Machar, baada ya kushambuliana kwenye jimbo la Upper Nile.Nini kinaweza kufanyika kuzuia mzozo mpya ?Wachambuzi wetu ni Dokta Brian Wanyama, kutoka Kenya na Hamdum Marcel akiwa Mwanza, Tanzania.
-
Serikali ya umoja wa kitaifa itasuluhisha mzozo wa DRC ?
12/03/2025 Duration: 10minWakati huu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, inapoendelea kukabiliwa na changamoto ya usalama Mashariki mwa nchi hiyo, baada ya waasi wa M23 kuingia katika miji ya Bukavu na Goma, rais Felix Tshisekedi ametangaza mpango wa kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuwashirikisha wanasiasa wa upinzani.Tunajadili iwapo hatua hii itasaidia kutatua mzozo wa mashariki mwa DRC.
-
Je, Raila ataegemea upande gani wa kisiasa ?
05/03/2025 Duration: 09minKiongozi wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga , yupo kwenye harakati za mashauriano ya kisiasa na wafuasi wake, kabla ya kutangaza mustakabali wake wa kisiasa baada ya kukosa uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Je, Raila ataegemea upande gani ? Tunachambua.
-
Hatima ya mzozo wa Sudan baada ya RSF kusaini mkataba wa kuunda serikali mbadala
26/02/2025 Duration: 09minWajumbe wa kisiasa kutoka kundi la RSF linaloongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo linalopigana na wanajeshi wa Sudan, walikutana jijini Nairobi na kutia saini mkataba wa uundwaji wa serikali mbadala kwenye maeneo wanayodhibiti. Nini hatima ya mzozo wa Sudan ?