Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

Wakaaji wa mijini wanavyotumia Bustani ya Nyumbani kukabili mabadiliko ya tabia nchi

Informações:

Synopsis

Utunzaji wa bustani ya nyumbani, ni mbinu mpya ya kilimo inayolenga kutimiza malengo matatu kwa wakati mmoja: kuongeza mapato ya kilimo, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuimarisha ustahimilivu, halkadhalika kupunguza uzalishaji wa gesi chafuzi. Bustani ya Nyumbani, kwa kawaida huwa karibu na jikoni au pia kwenye roshani. Bustani hii ambayo mara nyingi hutumia mbolea asilia husaidia kupambana na mabadiliko ya tabianchi kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu na pia kutunza udongo.Bustani hii hutumika kwa kilimo cha mboga, viungo vya upishi kama vitunguu, matunda, au mimea ya kitiba kwa matumizi.