Afrika Ya Mashariki

Namna wakazi wanaoishi karibu na migodi wanaweza kufaidika na shughuli hizo

Informações:

Synopsis

Makala ya Afrika mashariki hii leo tunatuwama na kuangazia kwa namna gani wakazi wanaozunguka migodi ya madini kupitia uwajibikaji kwa jamii. Mchango wa Sekta ya Madini katika Pato la Taifa umekua, na kukua huku ni kutokana na ongezeko la asilimia 7.3 kwa mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 9. Kwa kuzingatia umuhimu wa sekta hii serikali ya Tanzania imechukua hatua muhimu ya kuhakikisha kwamba wawekezaji wakubwa na wadogo kwenye Sekta ya Madini wanaendesha shughuli zao kwa tija kwa kuwezesha mazingira wezeshi ya uwekezaji na upatikanaji teknolojia unaimarika, hii ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ambayo serikali imeamua kuimarisha kwa lengo la kuvutia uwekezaji na kuwezesha uwekezaji huo kuleta faida kwa kila mwekezaji.